Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 5, 2016

ZINEDINE ZIDANE KUIFUNDISHA MADRID BAADA YA BENITEZ KUFUKUZWA

Zinedine Zidane akiwa na Rais wa Madrid Fiorentino Perez mara baada ya kutangazwa kuwa kocha wa muda wa klabu hiyo.
Klabu ya Real Madrid imemtangaza mchezaji wake wa zamani, Zinedin Zidane (Zizou) kuwa kuwa kocha wa muda wa timu hiyo na kuchukua nafasi ya Rafael Benitez aliyefukuzwa  kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Zidane amekuwa kocha wa Real B tangu mwaka 2014,  Kabla ya hapo alikuwa mwanachama muhimu na baadae akawa katika jopo la ufundi chini ya kocha Carlo Ancelotti, ambaye aliiongoza Madrid kuchukua Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10.

Benitez mwenye umri wa miaka 55 amefukuzwa kwenye klabu hiyo mara baada ya mkutano wa bodi ya klabu hiyo siku ya Jumatatu na amefukuzwa nikiwa ni miezi saba tu, tangu alipopewa jkumu la kuifundisha timu hiyo.