Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 11, 2016

MESSI AIPAISHA BARCELONA KILELENI

Mshambuliaji Lionel Messi ameibeba Barcelona baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo dhidi ya Granada na kuiwezesha timu yake kurudi kileleni mwa ligi ya La Liga.

Raia huyo wa Argentina alifunga mara mbili katika dakika 15 za kwanza na kuongeza bao jingine baada ya mda wa mapumziko hivyo basi kuongeza idadi ya mabao aliyofunga kufikia 18 huku Barcelona ikifaulu kucheza mechi 20 bila kupoteza.

Messi aliiweka Barcelona kifua mbele baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa mshambuliaji matata wa timu hiyo Louis Suarez na aliongeza bao la pili katika dakika ya 58 kabla ya Neimar kufunga bao la nne.