Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 11, 2016

ARSENAL, MAN UTD, MAN CITY ZASONGA MBELE FA CUP


Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Arsenal wamefanikiwa kufuzu kwa raundi ya tatu baada ya kufanikiwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya Sunderlan.

Sunderland ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya  Jeremain Lens kufunga bao akiwa ndani ya boksi baada ya beki Laurent Koscielny kuzembea kuokoa mpira.

Baadae  Arsenal ilisawazisha kupitia Joel Campbel na baadaye Aaron Ramsey akaongeza bao la kisha mshambuliaji Olivier Giroud kufunga bao la tatu na kufanya mchezo kumaliziaka kwa mabao 3-1.

Kwa upande wa Man City,  Sergio Aguero aliiongoza timu hiyo kupata ushindi dhidi ya Norwich City baada ya kufunga bao na baadae kutengeneza bao lingine lililofungwa na  mshambuliaji kutoka Nigeria Kelechi Iheanacho.

City ilitawala mchezo na haikuchukua mda mrefu Kevin De Bruyne alipofunga bao la tatu na kuhitimisha ushindi wa mabao 3-1.

Nayo Manchester United ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Sheffiled United,bao lililofungwa kwa njia ya penalti na nahodha Wayne Rooney baada ya Memphis Depay kuangushwa katika eneo la hatari zikiwa zimebaki dakika chache mpira kwisha.