Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 13, 2016

WAHAMIAJI WANAOINGIA NCHINI BILA KIBALI WAENDELEA KUKAMATWA KIGOMA

Idara  ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma inaedelea na zoezi la kukamata wahamiaji wanaoingia nchini bila kibari mara baada ya kushamili kwa wimbi la raia wa kigeni kukimbilia nchini kutokana na machafuko nchini mwao.

Sakata la wakimbizi kuingia nchini lilianza mwanzoni mwa mwaka 2014 baada yamachafuko katika nchi ya Burundi ambapo raia hao walikuwa wakipokelewa katika kijiji cha Kagunga na kwenda kuhifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu.

Akizungumza na gazeti hili hii leo, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma Naibu Kamishina  Maurice Kitinusa, amesema, wahamiaji bado wanaendelea kuingia nchini japo si kwa kiwango kikubwa kama ilivyokuwa mwaka jana.

Amesema, kati ya wahamiaji wanaoingia nchini wapo wanaofuata sheria kwa kupitia katika ofisi za uhamiaji zilizoko mipakani na wengine huingia kinyume cha sheria kwa kupita njia zisizo rasmi.

“Hao wanaoingia kinyume cha sheria ndio tunaowasaka na kuwakamata na zoezi linafanyika kila siku mana kila siku wanaingia wahamiaji wapya hivyo na sisi tufanya zoezi hilo kila siku” amesema Kitinusa.

Aidha Kitinusa amesema, raia wanaokamatwa ni wale wanaoingia nchini kinyume cha sheria sambamba na wale wanaotoroka makambini na kuingia kwenye makazi ya watu bila kufuata sheria.

“Suala la wakimbizi kurotoka makambini na kuingia kwenye makazi ya watu kwa asilimia kubwa linachangiwa na watanzani ambao huwachukua na kuwaajiri katika mashamba yao, na tunapobaini uwepo wa wahamiaji eneo furani huwa tunawakamata sambamba na waajiri wao hata kama ni watanzania lakini nao huchukuliwa hatua za kisheria mana ni makosa kumtumikisha mhamiaji kinyume na sheria” amesema Kitinusa.

Hata hivyo Kitinusa amesema, tangu kuanza kwa zoezi la kukamata wahamiaji hao mpaka sasa walishakamata wahamiaji wengi ambapo takwimu sahihi ataitoa siku ya ijumaa baada ya kufanya majumuisho kwa kila wilaya mkoani hapa.

“Mpaka Ijumaa tutakuwa tumeshakamilisha idadi kamili ya wahamiaji tuliowakamata pia baada ya kukamilika ndio nitawaambia kuhusu maamuzi yanayochukuliwa dhidi yao kama ni kuwapeleka mahakamani au kuwarudisha nchini kwao” amesema Kitinusa.