Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 14, 2016

REAL MADRID NA ATLETICO MADRID ZAFUNGIWA KUSAJIRI WACHEZAJI WAPYA

Klabu hasimu nchini Hispania Real Madrid na Atletico Madrid zimepigwa marufuku kutonunua wachezaji wapya katika vipindi viwili vya usajiri.

Klabu hizo zimeadhibiwa na shirikisho la soka duniani Fifa kwa kukiuka sheria za uhamisho wa wachezaji kutokana na  kununuliwa kwa wachezaji ambao bado ni watoto.

Kifungu hicho hakitaathiri kipindi cha sasa cha usajiri ambacho kinaendelea hadi mwisho wa mwaka huu.

Atletico pia wametozwa faini franka 900,000 za Uswizi ambazo ni sawa na pauni 622,000 za Uingereza, nao Real wakatakiwa kulipa franka 360,000 (£249,000).