Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 13, 2016

VAN GAR AJITETEA BAADA YA KUTOKA SARE YA 3-3 NA NEWCASTLE

Baada ya klabu ya Manchester United kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya  Newcastle  kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal amesema klabu yake ilikuwa na nafasi ya kufunga mabao sita katika mechi hiyo.

Van Gaal amesema kuna wakati mwingine amekuwa hapendezwi na uchezaji wa timu yake lakini kwenye mechi hiyo walicheza vyema na nusura waondoke na ushindi lakini Paul Dummett akasawazishia wenyeji dakika za mwisho.

“Bila shaka ninahisi ni kama tulishindwa. Tulitupa ushindi,” alisema Mholanzi huyo ambaye vijana wake wakati mmoja waliongoza 2-0.

"Tungefunga mabao sita lakini lazima ufunge bao moja zaidi ya mpinzani wako, Vijana wangu walishambulia sana dakika za kwanza 45 na Wayne Rooney alifunga penalti na kisha akasaidia Jesse Lingard kufunga la pili jambo lililonifanya niamini kuwa nitaondoka na pointi tatu" alisema Van Gar.
Tofauti na alivyokuwa akiamini Van Gar, Newcastle walisawazisha kupitia Georginio Wijnaldum na Aleksandar Mitrovic, Rooney aliwarejesha tena mbele lakini Lingard na Marouane Fellaini walipoteza nafasi murua za kufunga kabla ya Dummett kusawazisha.

“Tulitupa ushindi, nimewaambia hivyo wachezaji wangu,” Van Gaal ameongeza.
Aidha Van Gar  alikosoa uamuzi wa refa wa kutoa penalti baada ya Chris Smalling kudaiwa kumchezea vibaya Mitrovic, penalti ambayo mshambuliaji huyo alifunga na kusawazisha.

"Refa alitoa penalti na hakukuwa na kosa lolote, ni wachezaji wawili walikuwa wanakabiliana, na huwezi kuamua ni nani amemfanyia mwingine madhambi.” alitetea Van Gar.
Georginio Wijnaldum alifungia Newcastle bao la kwanza