Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari mkoani Kigoma wamezungumzia chamgamoto zinazowakabiri baada ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzuia michango kwa wazazi kwa lengo la kutoa elimu bure.
Wakizungumza
blog hii Wakuu wa shule hizo wamesema, Changamoto hizo zimeanza kuonekana baada
ya serikali kutoa pesa kwa kila shule ambapo uchache wa pesa hizo unasababisha kushindwa
kukidhi mahitaji ya shule zao kama ilivyokuwa awali.
Thomas
Masama ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru iliyoko Halmashauri ya
Wilaya ya Kasulu Mjini, amesema, tangu kuzuiliwa kwa michango ya wazazi
shughuri mbambali za uendeshaji wa shule umekuwa mgumu kutokana na pesa
zilizotolewa kuwa chache.
Amesema,
kwasasa wanashindwa kununua vifaa vya shule, kuendesha vikao vya bodi sambamba na
kuwalipa walinzi mishahara yao pia bado shule ina madeni ambayo
ilichukua vifaa kipindi pesa hazipo.
“Shule
yangu ilipewa Tsh. 286,000/= ambapo pesa hiyo haitoshi kulingana na mahitaji
tuliyonayo na kwa wingi wa wanafunzi nilionao ambao ni 540 ilitakiwa nipewe kiasi cha Tsh. 5,040,000/=
kwani Waziri wa Elimu alisema kila mwanafunzi analipiwa Tshs, 10,000/=” alisema
Mwalim Msama.
Nae
Mkuu wa Shule ya Sekondari Hwazi,
Jonathan Nkundike, amesema, baada ya michango kufutwa na kupokea pesa kutoka
serikalini changamoto kubwa inayoikumba shule yake ni kushindwa kuwalipa
mishahara wasaidizi na walinzi wa shule ambao waliajiriwa na shule.
Ameongeza
kuwa, katika uendeshaji wa shule kuna vifaa mbalimbali huwa vinahitajika
sambamba na uendeshaji wa vikao vya bodi
hivyo kwasasa wanashindwa wafanye kipi kutokana na pesa kuwa chache
kutokana na mahitaji ya shule kwa ujumla.
“Tunaweza
kusema tununue vifaa vya shule ambavyo
ni muhimu ila bado vikao vya bodi navyo
ni muhimu mana bodi ya shule ndio imepewa dhamana ya kusimamia pesa hizo
pia walinzi na wasaidizi wa shule wanadai
pesa zao na mwisho wa siku wataondoka mana hawawezi kufanya kazi bila kulipwa
hivyo shule inaweza kubaki bila walinzi na wasaidizi” amesema Nkundike.
Hata hivyo walimu hao wameitaka serikali
kuangalia upya suala hilo na kama imedhamilia kutoa elimu bure basi itoe pesa
za kutosha sambamba na kutoa vifaa vya shule kama madaftari, chaki,
vitabu, pia kutenga mishahara kwaajiri ya walinzi wa shule ili kutatua
changamoto zinazozikabili shule hizo baada ya michango kufutwa.