Waziri wa habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye. |
Kauli
ya serikali ya kuzuia vipindi vya bunge kurushwa moja kwa moja kwenye runinga
imepokewa kwa muono tofauti na wakazi wa Kigoma baada ya kuonekana haina tija
kwa wananchi.
Wakitoa
maoni yao kwa nyakati tofauti wananchi hao wakiwemo viongozi wa dini
mkoani humo wameonyesha kutoridhishwa na kauli ya serikali inayoelekea kuwanyima wananchi
uhuru wa kupata habari kwa muda muafaka.
Shaban
Guoguo ambaye ni Shekhe Mstaafu wa Mkoa wa Kigoma, amesema, kilichoamuliwa
na serikali ni upindishwaji wa sheria mana bunge ni la wananchi na sio la
serikali hivyo wananchi wanataka kuona wabunge wakiwasilisha yale waliyowatuma.
Amesema, kama serikali inatambua bunge ni la wananchi na yanayozunguzwa humo ni
kwaajiri ya kutetea taifa basi mambo yote yawe wazi na kama wanaamua kuzuia
wananchi wasione basi haina haja kuwa na bunge mana itaonekana yanayozunguzwa
humo ni maovu hivyo wanayaficha yasionekane na wananchi.
“Serikali
inataka kuleta mgogoro usio na sababu, kama bunge linavurugu, wabunge hawaelewani
na nidhamu haipo mbungeni, dawa si kuzuia wananchi wasione mana kuzuia si
kutatua tatizo mana sasa kama wamezuia kabisa itafika siku wabunge watapigana
kabisa mana wanajua hawaonwi na waliowatuma” amesema Shekhe Guoguo.
Nae
Mthibiti Ubora wa Shuke mkoani Kigoma,
Romward Nyuki amesema, serikali imeamua kuvunja haki ya binadamu ya kupata taarifa sahihi mana lengo lao ni
kuonyesha vipindi vilivyo recodiwa ambavyo kimsingi vinakuwa vimechunjwa kwa
kuondoa mabaya yote.
Amesema, bunge linakaa kwa masaa manane kwa siku ila serikali inataka matukio
yote yaonyeshwe kwa saa moja ambapo itawalazimu kuondoa vitu vingi jambo
ambalo litaua dhana nzima ya wananchi kufahamu kinachoendelea bungeni.
“Serikali
itambue kuwa ikiendelea kung’ang’ania suala hilo basi ijue wananchi watapoteza
imani na serikali yao na kuamini kuwa bunge halipo kwaaajiri ya masrahi ya
wananchi bali kwa masrahi ya watu wachache” amesema Nyuki.
Gidion
Ruhadha ambaye ni Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mnarani, amesema, serikali
inatakiwa kutambua matokeo ya kauli yake kama yanafaida kwa taifa au kwa watu
wachache hivyo jambo la msingi ni kujali mahitaji ya wananchi .
“serikali
inayoongozwa na sera ya ukweli na uwazi ndio hufanikiwa mana hutoa uhuru kwa
watu wote kufahamu mambo yanayoendela katika nchi yao sasa kama wameamua
kuficha basi hatuna budi kusema wanataka wapate fursa ya kuwagandamiza wananchi
ili wajinufaishe wenyewe” amesema Ruhaza