Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 28, 2016

MABOMU MAWILI YAOKOTWA KIGOMA



Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui.
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limeokota mabomu mawili aina ya Rocket ya kurushwa kwa ndege katika maeneo mawili tofauti ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Januari 26.

Akizungumza na blog hii, Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, SACP Ferdinad Mtui alisema kuwa, bomu la kwanza liliokotwa katika Kata ya Kitongoni Ujiji majira ya saa 7 mchana.

Alisema kuwa, bomu la pili liliokotwa siku hiyo hiyo maneneo ya Forodhani ujiji majira ya saa 11 jioni na aliongeza kuwa mabomu hayo yaba uzito wa Kg 13 na ukubwa wa mm 35 ambayo hutumika kwa kutungulia ndege.

Hata hivyo Kamanda Mtui aliwataka wananchi kutokuchezea vyuma wanavyoviona sehemu yoyote bila kujua matumizi yake bali watoe taarifa polisi.