Wananchi
mkoani Kigoma wametakiwa kuachana na tofauti za kiitikadi zilizojitokeza
kipindi cha uchaguzi uliofanyika Octoba 25 mwaka jana na kuungana na serikali
iliyopo madarakani katika kuiombea
utumishi uliotukuka.
Akizungumza katika mkutano wa kumshukuru Mungu kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi
kuisha kwa amani na utulivu uliofanyika Desemba 30, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa
Machibya alisema, wananchi wote wanatakiwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania John Magufuri kwa
kauli yake ya HAPA KAZI TU kwa kufanya
kazi kwa bidii kama anavyoagiza.
Alisema,
wananchi wote wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa viongozi mbalimbali
waliochaguliwa kuanzia ngazi ya mtaa, kata, Wilaya na Mkoa bila kujari tofauti
za kiitikadi, kidini na kikabila.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akizungumza na wananchi katika ibada ya kumshukuru Mungu iliyofanyika katika viwanja vya Community Centre katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji. |
Aidha
Machibya aliwataka wananchi kuendelea na utulivu ili Tanzania iendelee kuitwa
kisiwa cha amani badala ya kuanzisha fujo ambazo zitapelekea kuipoteza amani
ilipo.
“Nahitaji
wananchi wote muelewe kuwa huu sio muda wa marumbano bali ni muda
wa kufanya kaza kwa bidii kwa lengo la kuziendeleza familia zetu na nchi kwa
ujumla” alisema Machibya.
Akisoma
risala kwa niaba ya Umoja wa Makanisa ya Kikristo (CPCT) mkoa wa Kigoma, Askofu Mstaafu wa Kanisa la Pentekoste Assembless Of God
Tanzania (P.A.G.T.) Kigoma, Michael Kulwa, alisema kuwa, amani iliyoko sasa
mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi inatokana na utulivu wa watanzania
sambamba na maombi ya wakristo waliojitoa kuuombea uchaguzi uishe kwa amani.
Kulwa
alisema kuwa, ni wakati sasa kwa viongozi wote wa idara mbalimbali, wanasiasa
na wananchi wote kwa ujumla kuwa, sasa uchaguzi umekwisha, ni vyema wote
kuungana kwa pamoja na kuwa kitu kimoja kwa kutunza amani ya nchi na kutekeleza
yale yanayoagizwa na Rais Magufuri.
“Tunafahamu
kuwa Watanzania wote wanajua yanayotokea nchi za jirani mara wanapomaliza
chaguzi zao ambapo amani hutoweka na nchi kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe
hivyo ni vyema sisi watanzania kuendelea kumuomba Mungu azidi kutupa moyo wa
upendo kwa kila mmoja wetu ili amani iendelee kudumu” alisema Askofu Kulwa.