Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, akizungumza na wanannchi alipokuwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kigoma. |
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amekemea tabia ya
Mamlaka ya Usafirishaji wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) ya kuwatoza wavuvi
ushuru kwa njia ya dora.
Akizungumza
na wavuvi baada ya kufungua soko jipya la samaki, liloko Kata ya Kibirizi
katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani hapa, Waziri Mkuu alisema, licha ya
kupokea malalamiko kutoka kwa wavuvi kuhusu tozo ya dora suala hilo ni kinyume
na sheria.
Alisema,
tozo la dora hufanyika kwa watu ambao si raia wa nchi hii lakini kwa Watanzania
wote wanatakakiwa kutumia pesa ya Kitanzania ambayo ni rahisi kupatikana.
Aidha
Waziri Mkuu aliitaka SUMATRA kuacha tabia hiyo ili kuepusha migogoro isiyo na
tija baina yao na Wananchi.
Awali
wavuvi wanaotumia Ziwa Tanganyika walilalamikia usumbufu wanaoupata wa
kubadirisha pesa za Kitanzania kuwa dora ili kulipia ushuru baada ya kutakiwa
kufanya hivyo na SUMATRA.
Hata
hivyo Waziri Mkuu alimaliza Ziara yake ya siku tatu mkoani kigoma hapo jana
ambapo alitembelea Wilaya tatu ikiwemo Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo.