Ziara
ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, mkoani
Kigoma imewaacha matatani baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma Ujiji, baada ya kubaini uuzwaji wa majengo ya Halmashauri kinyume na
taratibu.
Majengo
hayo ni pamoja na jengo la Kigodeco, Jengo la Mwanga Center, viwanja 16 pamoja
na msitu wa masanga, hali iliyosababisa Waziri Mkuu kutoa agizo kwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi John Ndungulu kusimamie mchakato wa
ufuatiliaji wa tuhuma hizo mpaka itakapofika Januari 2, 2016 ambapo
atatakiwa kuwasilisha ripoti katika ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu Majaliwa alitoa kauli hiyo hii leo kwenye kikao cha majumuisho ya ziara
yake ya siku tatu mkoani humo katika ukumbi wa NSSF, ambapo alisema
kuwa uchunguzi unaonyesha uuzwaji wa mali hizo za umma haukuwa wa kiharari.
Awali
uzwaji wa majengo ulisitishwa na uongozi wa Mkoa kwa kuwa mali hizo ni sehemu
ya mali ya umma, lakini licha ya kusitishwa huko Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kigoma Ujiji, Boniface Nyambele kwa kushirikiana na madiwani wa
Halmashauri hiyo waliuza mali hizo.
“Leo
Mkurugenzi na Mhandisi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mtaenda kwa Katibu Tawala wa
Mkoa na kutoa maelezo kwa maandishi kuhusu mchakato mzima wa uuzwaji wa majengo
na viwanja hivyo kwa bei ya kutupa” aliagiza Waziri Mkuu Majaliwa.
Baadhi ya viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani hapa. |
Aidha
baadhi ya Madiwani walikuwa katika mchakato huo Asha Omari na Mgeni Kakolwa kwa
nyakati tofauti walikiri majengo kuuzwa kwa utashi wa Mkurugenzi wa
Halmashauri akishirikiana na aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyo Bakari Beji
na Naibu wake Rashidi Ruhomvya.
“Mwezi
wa saba tuliitwa katika kikao cha dharura lakini ajenda za kikao
hatukuzifahamu, baada ya kuingia tukakuta ajenda ya kuuzwa kwa mali hizo,
tulivutana baina ya madiwani wa CCM na
CHADEMA, lakini kwakuwa madiwani wa CCM tulikuwa wachache ajenda hiyo
ilipitishwa na kuuzwa kwa mali hizo za
umma” walibainisha Madiwani hao.
Kwa
mujibu wa madiwao hao, jengo la Kigodeco liliuzwa kwa kiasi cha shilingi
milioni 375 ambapo katika fedha hizo,kiasi cha cha milioni 167
zirirudishwa kwa mzabuni aliyekuwa amekodisha jengo hilo baada ya kukatisha
mkataba na sh.milioni 100 walidai wanawekeza katika ujenzi wa maabara wa shule
za skondari za manispaa hiyo.
Wakati
huohuo kiongozi mmoja wa manispaa hiyoambaye hakupenda jina lake litajwe
alisema kuwa, skendo hiyo ina mikono mingi ,kwa kuwa mkurugenzi hawezi
kuuza bila kushirikiana na wenzake ambao walianzisha mchakato huo na shida
kubwa ni kutokana na utashi wa siasa.