Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, SACP Ferdinand Mtui. |
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kigoma limetakiwa
kutatua kero ya ukosefu wa vyoo katika kituo cha ukaguzi wa magari kilichopo
njia panda ya Mwandiga ambapo huwalazimu askari kujisaidia vichaka mara
wanapohitaji kufanya hivyo.
Akizungumza
na blog hili hapo jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha NRA Taifa,
Fadhili Kiswaga , alisema kuwa, Askali
hufanya kazi ya kulinda raia na mali zao jambo ambalo huwafanya baadhi ya
Askali kuwa katika maeneo magumu.
Alisema
kuwa, eneo la njia panda ya Mwangida ni eneo muhimu sana kwa magari kukaguliwa
kutokana na njia hiyo kuwa ya kutoka na kuingia mkoani Kigoma ambapo Askali waliweka kituo kwaajiri
ya ukaguzi hivyo Askali huwepo eneo hilo masaa 24 ili kukagua usalama wa magari
yanayoingia na kutoka.
“Licha
ya kuwa eneo hilo ni muhimu sana na askali huwepo muda wote lakini eneo hilo
halina vyoo kwaajiri ya kujisaidia pindi askali wanapotaka kufanya hivyo,
kukosekana kwa vyoo huwafanya askari kujisadia vichakani na kwenye mashamba ya
watu” alisema Kiswaga.
Aidha
Kiswaga alisema kuwa, kitendo cha askari katika kituo hicho kujisaidia
vichakani ni cha uzalilishaji na kinaonyesha jeshi la polisi haliwajari askali
wake wanapokuwa katika maeneo ya kazi.
“Jeshi
la polisi linatakiwa kujenga vyoo katika eneo hilo ili kuonyesha linawajari
askali wake wanapokuwa katika maeneo ya kazi” aliongeza Kiswaga.
Alipoulizwa
kuhusu kero za vyoo katika eneo la njia panda ya Mwandiga, Kamanda wa Polisi
mkoani Kigoma, SACP Ferdinand Mtui, alikili kuwepo kwa kero hiyo na aliongeza
kuwa atazungumza na wahusika wa utawala ili kutatua kero hiyo kutokana na kituo
hicho kuwa kikubwa.
“Nawataka
Askali waendelee kuzingatia kanuni na sheria za kazi kwa kuhakikisha wanafanya ukaguzi kwa magari yanayoingia na
kutoka mkoani hapa na suala la vyoo litafanyiwa kazi ili huduma hiyo ipatikane
haraka iwezekanavyo” alisema Kamanda Mtui.
Kwa
upande wa baadhi ya Askari wa usalama barabarani ambao hukaa katika kituo
hicho cha ukaguzi, majina yao yanahifadhiwa, kwa nyakati tofauti walikili
kuwepo kwa tatizo la ukose vyoo linalowasumbua kwa muda mrefu sasa.