Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Feb 7, 2016

LEICESTER CITY HAWAKAMATIKI ENGLAND

Klabu ya Leicester imeendeleza ubabe wake na kuendelea kuongoza ligi kuu nchini England baada ya kuwafunga wapinzani wake wa karibu katika ligi katika mbio za ubingwa  Manchester City baada ya kuwacharaza 3-1 katika uwanja wa Etihad na kuonngeza pengo la pointi baina yao.

Beki Robert Huth alifunga bao la kwanza baada ya kona iliopigwa na nyota wa timu hiyo Mahrez ,likiwa ni bao lililoiweka kuiweka kifua mbele timu yake.

City ilitishia kusawazisha bao kwa kuvunja safu ya ulinzi ya Leicester huku mabeki wao wakionekana kutatizwa na washambuliaji wa Leicester.
Mahrez alifunga bao la pili huku Huth akifunga bao la tatu na kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ya Sergio Aguero kuipatia City bao la kufutia machozi kunako dakika za mwisho.

Leicester ilikuwa imeishinda Tottenham iliopo katika nafasi ya tatu lakini ni ushindi huu dhidi ya Manchester City ambao umekuwa muhimu sana kwao.

Mbweha hao sasa wamechukua pointi 28,licha ya kupokonywa ushindi wa sita katika mechi zao saba.