Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jul 5, 2015

CHILE MABINGWA COPA AMERICA WAIFUNGA ARGENTINA

Timu ya Taifa ya Chile imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Copa Amerika baada ya kuwashinda Argentina kupitia kwa mikwaju ya penalti na limekuwa  kombe la kwanza la kimataifa kuwahi kushindwa na Chile.

Chile ambayo walikuw awenyeji wa mashindano hayo, waliwashinda Argentina mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu zote kukosa kufunga.

Ni miaka 22 tangu Argentina washinde kombe lolote kubwa kwenye mashindano ya kandanda ya kimataifa.

Mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain kupiga nje huku mkwaju wa Ever Banega ukinyakwa na kipa Claudio Bravo.
Awali Higuain alikuwa amekosa bao la wazi aliposalia na kipa baada ya dakika 90 za mchezo na Sanchez alikaribia kufunga katika dakika za ziada lakini mpira haukuingia wavuni.


 Miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliojaa kuishabikia timu yao ni wachimba mgodi 33 waliokwama chini ya mgodi kwa wiki kadhaa mwaka 2010,katika kisa kilichovutia hisia nyingi duniani.