Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jun 21, 2016

WANAFUNZI WALAZIMIKA KUSOMEA MSIKITINI


Picha haihusiani na Sehemu inayozungumziwa
Kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, wanafunzi wa shule ya msingi Nyantole iliyopo kitongoji cha Nyantole kata ya Ziwani Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamelazimika kusomea katika jengo la msikiti kwa miaka mitatu sasa.     
 
Wanafunzi hao wamelazimika kuchangia jengo la msikiti pamoja na watoto wa madrasa huku wakiingia asubuhi na madrasa wakianza elimu yao ya dini majira ya mchana.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyi, Magese Ngasa na Chausiku Hussein ambaye ni mwanafuzi wa shule hiyo wameelezea adha wanayoipata kutokana na kukosa vyumba vya madarasa huku wakiitaka serikali kuwasaidia vyumba vya madarasa 

Aidha shule hiyo inakabiliwa na tatizo la upungufu wa matundu ya vyoo huku yaliyopo ni matundu mawili yanayotumiwa na wanafunzi 184 pamoja na walimu wao jambo linasababisha wanafunzi wengine kujisaidia vichakani.

Diwani wa kata hiyo Zuberi Maftaha amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kuiomba jamii kujitokeza kuchangia nguvu zao ili kufikia lengo la uhitaji wa madarasa matano yatakayokidhi mahitaji ya wanafunzi hao.

Kwa upande wake, Mkurugrnzi wa Halashauri ya Wilaya ya Kigoma Michael Mwandezi amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuongeza kuwa serikali inajipanga kutatua changamoto hiyo.