Serikali
imetakiwa kujenga miundombinu katika mpaka uliopo kata ya Muyama Wilaya
ya Buhigwe mkoani Kigoma na nchi jirani ya Burundi hasa soko la ujirani mwema ili kuwawezesha
wananchi kuuza na kufanya biashara zao kwa uhuru na kujiletea maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Muyama, Abdala Moshi wakati
akizungumza na Radio Joy ambapo amesema kutokana na Kata a Muyama kuwa mpakani
mwa nchi ya Burundi kumepelekea raia wa nchi hizi mbili kuwa na muingiliano wa kibiashara.
Amesema
endapo serikali ikijenga soko la ujirani mwema litatoa fursa kwa watanzania wa
kata hiyo kuuza bidhaa zao kwa wingi na kujiingizia kipato pia kuingizia nchi
pesa za kigeni.
Hata
Hivyo Moshi alisema awali kulikuwa na mkakati wa kutengeneza soko la ujilani mwema
kabla ya Wilaya ya Buhigwe kupewa hadhi ya Wilaya lakini mkakati huo ulikwama
baada ya kugawa Wilaya.
Kwa
upande wao wananchi wa kata hiyo, akiwemo Abu Ahmad na Ndimugwanko Gwimo waliitaka serikali kuboresha soko lililopo ili kutoa fursa kwao kuuza bidhaa
nyingi jambo litakalowafanya kujiingizia kipato.