Wakazi wa mkoa wa Kigoma waishio
mwambao mwa ziwa Tanganyika wameupongeza mradi wa TUUNGANE kwa hatua uliyofikia
katika kusimamia utunzaji wa mazingira ya mlima wa Hifadhi ya Mahale pamoja na
ziwa Tanganyika yaliyokuwa yakiharibiwa na wakazi hao kutokana na ukosefu wa
elimu.
Mradi huo wa TUUNGANE unaotekelezwa
na shirika la la Pathfinder international na the nature conservancy unaolenga
utunzaji wa mazingira na afya umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 mkoani
Kigoma katika milima ya hifadhi ya mahale na Ziwa Tanganyika kutokana mbinu
mbalimbali zilizotumika katika utekelezaji wake.
Wakizungumza na blog hii
mkoani humo, Lukasi Kanoni na Lusia Mathias ambao ni wakazi wa Kalya walisema
kuwa, mradi huo umefanikiwa kutokana na kuwa njia iliyotumika katika
utekelezaji wa wake ilikua shirikishi ambapo mazoezi ya utunzaji mazingira
yalifanyika kwa vitendo.
“tuwapongeze wasimamizi wa mradi kwa
hatua hii waliyofikia, tulifundishwa kwa vitendo kama namna maji ya ziwa
yanavyochafuliwa na vinyesi kutoka vichakani kwa wakazi wasio na vyoo, lakini
tulifundishwa kutochoma msitu katika maeneo yetu” alisema Mathiasi
Meneja mradi Petro Masolwa alisema,
mradi unatekelezwa wilayani Uvinza mkoani Kigoma ambapo lengo ni kutunza
mfumo wa Ikolojia ya Milima ya Mahale na mazinira ya ziwa Tanganyika na kusema
kuwa mradi ulianza 2011 ukienda sambamba na masuala ya utengamano kati ya watu,
afya na mazingira yanayowazunguka.
Masolwa alisema kulinda ardhi na
misitu, maji na samaki wa ziwa Tanganyika, afya ya uzazi (nyota ya kijani),
pamoja na afya ya msingi ni moja ya malengo ya mradi ambapo mpaka sasa
malengo hayo yameweza kutimia kwa asilimia 90 na mpaka sasa mikakati
iliyowekwa na mradi ni kuboresha utawala bora ngazi ya vijiji, usimamizi wa
rasilimali ardhi na misitu, uvuvi endelevu, pamoja na mawasiliano katika maeneo
hayo.
“tumefanya hivyo ili kupata urahisi
wa kazi ya utunzaji utekelezaji wa mradi, wakazi wa vijiji hivyo 24 walikua
wakikabiliwa na changamoto za huduma za kijamii ambapo tumetatua changamoto
hizo hivyo wakazi hao kutuunga mkono katika shughuli nzima” alisema Msolwa.
Afisa mawasiliano mradi Nelson Mmali
alisema, mradi umetoa mafunzo kwa vingozi wa vijiji na askali lengo ikiwa ni
kuwafanya watambue majumkumu yao ulinzi wa misitu na kwamba katika kutekeleza
huduma za kijamii zahati za vijiji hivyo zimekarabatiwa, mafunzo kwa wahudumu
wa afya yametolewa pamoja na kuweka miundo mbinu ya umeme wa jua.
Hata hivyo kutokana na vijiji hivyo
kukikabiliwa na changamoto ya magonjwa ya mlipuko usafi umehamasishwa ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa vyoo bora lengo ikiwa ni kuzuia kujisaidia vichakani
hali inayochangia uchafuzi wa maji ya Ziwa Tanganyika.
Iddi Ndabhona ambaye ni mwanasheria
wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma alisema wananchi wa Vijiji vya Sibwesa,
Buhingu, Kalya na Katumbi wametunga sheria ndogondogo zikiwa na lengo la
kuboresha uhifadhi wa mazingira pamoja na kuongeza kipato cha wakazi hao.
Ndabhona aliupongeza mradi huo na
kusema kuwa , kutokana na sheria hizo kufuata matakwa yote ya kisheria kikao
cha baraza la madiwani kilidhia kutumika kwa sheria hizo ambazo zinahusisha uhifadhi
wa mazingira na kudhibiti uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika.