Wafanyabiashara
wa dagaa Manispaa ya kigoma ujiji wameilalamikia serikali kwa kuongeza gharama za usafirishaji wa dagaaa kutoka Tsh
170 hadi Ths 2200 kwa kilo moja jambo linalofanya mauzo ya dagaa kushuka hasa
kwa mauzo ya nje ya nchi.
Wafanyabiasha hao wamesema serikali imefanya
maamuzi ambayo yanawakandamiza katika biashara kutokana na ongezeko hilo
kuwazuia wateja kutoka nje kushindwa kununua bidhaa hiyo.
Aidha
Wafanyabiashara hao wameitaka serikali kuwa na tabia ya kuwashirikisha wananchi
katika mabadiriko yanayogusa uchumi wao.
Akizungumzia
malalamiko ya wauza dagaa mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga amekiri kuwepo
kwa ongezeko la Gaharama za usafirishaji huku akiongeza kuwa Wizara ya Kilimo
Mifugo na Uvuni inafanya marekebisho baada ya kugundua ongezeko hilo
lilifanyika kimakosa.