Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Aug 11, 2016

MGAMBO FEKI WABAINIKA KIBONDO

Vijana wa Jeshi la Mgambo wakiwa kwenye mafunzo (Picha haihusiani na eneo la Tukio)
Wananchi wa kijiji cha nyaruyoba wilayani kibondo mkoani kigoma wameulalamikia uongozi wa kijiji kwa kuwapitisha baadhi ya watu kucheza mgambo ambapo hapo awali watu hao walikuwa wakimiliki sale za mgambo na kujiita kuwa ni wanamgambo.  

Diwani wa kata ya Nyaruyoba Bw charles Maseke amesema katika kata hiyo kuna watu wanao jiita kuwa wao ni wanamgabo huku wakiwa wamevaa sale za mgambo wakiwanyanyasa wananchi hivyo kuwa kero kijijini hapo.

Kwa upande wao wananchi wa Kata hiyo wamesema Vijana wanaojiita wanamgambo kijijini hapo wamekuwa wakifanya uharifu wa kutumia siraha kwa kuiba na kuvamia wanakijiji.


Nae  Mshauri wa Mgambo wiyalani kibondo meja Elisha Ndangula amesema wanafanya upelelezi kuhusu tuhuma hizo na endapo ikigundulika vijana hao watachukuliwa hatua.