Kijana ambaye alivamia nyuma ya Mwanamke mmoja na kutaka kumbaka, akiwa hajitambui baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira. |
Kufuatia
matukio ya baadhi ya wanawake kuingiliwa kimwili bila ridhaa yao nyakati za
usiku na watu wanaojulikana kwa jina la TEREZA Mtu mmoja ambaye jina lake
halijafahamika amekamatwa na Wananchi wakati akijaribu kumuingilia Mwanamke
mmoja katika kata ya Mwanga kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Akisimulia
tukio hilo Ramadhani Habibu mkazi wa mtaa wa Vamia katika kata hiyo ambaye
ndiye aliyepambana na TEREZA huyo amesema, Mtu huyo aliingia kwenye chumba cha
mke wa kaka yake na kutaka kumbaka lakini baada ya shemeji yake kupiga kelele
za kuomba msaada alitoka na kwenda kupambana na mtu yule.
“Baada
ya kusikia shemeji akiomba msaada nilitoka nikiwa na kipande cha nondo
nilipoingia chumbani kwa shemeji yangu nikamkuta mwanaume akiwa amevaa chupi tu
akitaka kumbaka na kwakuwa nilikuwa nanyemelea hakuniona ndio nikampiga na kile
kipande cha nondo shingoni” alisema Habibu.
Aidha
Habibu aliongeza kuwa baada ya kumpiga nondo mtu yule alipata mshituko hivyo
akatumia mwanya huo kupambana nae na baada ya muda majirani walikuja na kuanza
kumshambulia kabla ya Polisi kufika na kumpeleka kituoni.
Kwa
upande wa Mwanamke ambaye ndie alivamiwa
na mtu huyo amesema, kabla ya kulala alifunga mlango wa balazani lakini mlango
wa chumbani alisahau kuufunga na ilipofika saa kumi usiku TEREZA huyo akaingia
na kutaka kumbaka.
Kijana ambaye alivamia nyuma ya Mwanamke mmoja na kutaka kumbaka, akiwa hajitambui baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira. |
“Wakati
nimelala nilisikia mtu ananipapasa akinivua nguo ya ndani ndipo nikashtuka na
kumuuliza ni nani, akanambia nikae kimya ndipo nikaanza kupiga kelele za kuomba
msaada baada ya muda shemeji yangu akaja na kumpiga nondo hapohapo wakaanza
kupigana majirani walipokuja wote tukaanza kumpiga” alisema Mwanamke huyo.
Nae
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Mwamvita Jumanne aliitaka serikali kulihimiza jeshi la polisi kuwa na
utaratibu wa kufika mapema kwenye matukio ya uharifu baada ya kupewa taarifa
kutokana na wao kufika kwenye tukio saa 2 asubuhi wakati taarifa walipewa toka
saa 12 alfajiri.
Akithibitisha kukamatwa kwa Mtu huyo
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Naibu Kamishina Ferdinand Mtui amesema, baada
ya mtuhumiwa kukamatwa amefikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayomkabiri.