Baada
ya mganga mkuu wa Kituo cha afya Janda kutuhumiwa kuchukua zaidi ya shilling
millioni moja kinyumke na taratibu, mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Buhigwe ametakiwa kuchukua hatua dhidi ya mganga
huyo.
Mganga
huyo anaejulikana kwa jina la Dr.Froliani Asten anatuhumiwa kwa kugushi mhatasari wa kikao cha
bodi ya afya ya kata na kuchukua pesa ya mfuko wa afya ya jamii CHF ya kituo
hicho
Diwani
wa kata ya Janda Bw. Pascal Nkeyemba amezungumza
hayo na Radio Joy kwa njia ya simu na kusema kuwa mganga huyo aliwasahinisha
wajumbe wa bodi ambao si halali na pesa zilizochukuliwa zilikuwa kwa lengo la kununua
dawa ambazo hata hivyo hazikununuliwa.
Amesema
amekuwa akifuatilia suala hilo katika halmashauri ili hatua ziweze kuchukuliwa
lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika jambo ambalo limemfanya kumtaka
mkurugenzi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mganga huyo.
kwa
upande wake mkurugenzi wa wilaya ya Buhigwe Bw.Anosta Nyamoga amekili kuwepo kwa
tatizo hilo ambapo amesema limesababishwa na usimamizi mbovu katika kituo hicho
na ameunda tume kuchunguza suala hilo ambayo imekamilisha kazi yake na wakati wowote itatoa taarifa na hatua za
kisheria zitachukuliwa.
Nae
Mganga mkuu wa kituo cha afya cha Janda Dr. Frolian Asten amekanusha tuhuma
hizo na kueleza kuwa pesa hiyo ni ya muda mrefu na bado ipo kwa mkurugenzi ambaye
ndie mwenye taarifa zote.