Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Nov 11, 2016

DEREVA BODABODA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI KIGOMA


Askari wa Barabarani kwa kushirikiana na wananchi wakichukua mwili wa maerehemu baada ya kugongwa na gari hatimae kufariki papo hapo






Mtu mmoja ajulikanae kwa jina la Mranda Jumanne amefariki dunia baada ya kugongwa na gari eneo la Katubuka barabara ya kuelekea Airport Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Wakizungumzia tukio hilo lililotokea Novemba 9 majira ya saa 2 asubuhi,  Mashuhuda wa ajari hiyo wamesema, ajari hiyo imehusisha gari aina ya LandCruza na pikipiki ambapo dereva wa pikipiki alifariki papo hapo baada ya kugongwa.

Aidha Kamanda wa Jeshi  polisi mkoani hapa Naibu Kamishina Ferdinand Mtui amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo iliyosababisha kifo cha dereva huyo wa pikipiki.

Hata hivyo Kamanda Mtui amesema Dereva wa Gari lililosababisha ajari  alijaribu kukimbia lakini jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata na mpaka sasa yuko mahabusu.