Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Naibu Kamishina Ferdinand Mtui akiongea na waandishi wa habari |
Watoto
nane wamefariki Dunia katika kijiji cha Chakulu, Kata ya Uvinza Tarafa ya
Nguruka Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma baada ya nyumba waliyokuwemo kuungua
moto.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma, Naibu kamishina Ferdinand Mtui ametoa taarifa hiyo
mapema wiki hii ambapo amesema tukio hilo limetokea Septemba 4 mwaka huu majira
ya saa saba usiku wakati wazazi wa watoto hao wakiwa hawapo nyumbani.
Kamanda
Mtui amesema Nyumba iliyoungua ni mali ya Bw. Samike John ambaye ni mkazi wa
Kitongoji cha tandala eneo la kona nne
katika kijiji hicho pia kati ya watoto waliofariki wawili ni watoto wake huku
wengine wawili wakiwa ni wa dada yake sambamba na watoto watatu wa jirani yake.
Aidha
kamanda mtui amesema tukio hilo limetokea wakati wazazi wa watoto hao wakiwa
hawapo nyumbani ambapo moto huo ulisababishwa na jiko lililokuwa ndani.
Hata
hivyo kamanda mtui amewataka wazazi na walezi kujari maisha ya watoto wao kwa
kuwaaacha chini ya uangalizi wa watu wakubwa ili kuepusha matukio yoyote
yanayopelekea vifo na majeraha kwa watoto.