Baadhi ya wahamiaji waliokamatwa mkoani kikgoma wakiwa katika ofisi za uhamiaji mkoa. |
Baadhi ya wahamiaji waliokamatwa mkoani kikgoma wakiwa katika ofisi za uhamiaji mkoa. |
Idara
ya Uhamiaji mkoani Kigoma imekamata Jumla ya Wahamiaji haramu 1026 walioingia
na kuishi nchini kinyume cha sharia baada ya kufanya msako katika kipindi cha
mwezi April hadi Julai.
Akitoa
taarifa hiyo ofisini kwake hivi karibuni, Afisa Uhamiaji Mkoani Kigoma, Naibu Kamishina
Maurice Kitinusa, amesema Msako huo umefanyika katika wilaya zote mkoani hapa
na wahamiaji hao ni kutoka nchi za Burundi, Congo, Rwanda, Kenya, Msumbiji na
Uturuki.
Aidha
Kitinusa amesema katika idadi hiyo wapo watanzania ambao wao wamekamatwa kwa
kosa la kuwaficha wahamiaji sambamba na kuwazuia maafisa uhamiaji kufanya kazi
yao.
Ameongeza
kuwa, watanzania wenye nia ya dhati ya
kulinda nchi yao wanatakiwa kushirikaiana
na idara ya uhamiaji kwa kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali mara
wanapomuona mtu na kumtilia shaka pia amewataka watanzania kuacha kuwahifadhi
watu hao mana kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.