Zaidi kaya tisa katika kijiji cha Muyegela wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma hazina makazi ya kuishi mara baada ya kukumbwa na kimbunga kilali kilichoezua nyumba zao, kuharibu mazao sambamba na migugo kufa.
Wakazi hao akiwemo Silvesta Joseph amesema majira ya saa tano
asubuhi upepo mkali ulivuma kijijini hapo ambapo familia nyingi zilikuwa
mashambani huku wengine wakikubwa na upepo huo ambao uliezua mabati,
mifugo kufa,mazao kuharibika, nguo na vifaa mbalimbali vilivyokuwa ndani.
Aidha walitoa ombi kwa serikali ya kijiji na wilaya kuwasaidia
vifaa vya ujenzi ili wamudu kukarabati nyumba zao na waweze kuondokana na adha
wanazozipata za jua kali na mvua kutokana na nyumba zao kuezuliwa mabati.
Akitoa takwimu za uharibifu huo mtendaji Alphonce Ntatiye
amesema kutokana na tukio hilo wao kama serikali ya kijiji kwa kushirikiana na
wananchi wa maeneo hayo watashiriki kwa pamoja kuwapatia msaada waliokumbwa na
adhari za kimbunga kwenye kaya zao.
Hata hivyo kamati ya ulinzi na usalama ikiongonzwa na mwenyekiti
wa kamati hiyo mkuu wa wilaya Buhigwe kanal Marco Gaguti hakusita kutoa pole
kwa wakazi hao na kuahidi kuwapatia msaada ili wapate maeneo mazuri ya kuishi.