Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Nov 11, 2016

WATOTO WATATU WAFARIKI DUNIA KIGOMA


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kigoma Naibu Kamishina Ferdinand Mtui

Watoto watatu wanaosoma shule tofauti Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani hapa wamefariki dunia wakati wakiogelea katika ziwa Tanganyika Eneo la Lutare.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Naibu Kamishina Ferdinand Mtui amesema, tukio hilo limetokea Novemba 7 majira ya saa 12 Jioni wakati wanafunzi hao wakiogelea.

Kamanda Mtui amewataja majina watoto hao kuwa ni  Omary Ramadhani (11) mwanafunzi wa drs la sita shule ya msingi Kipampa, Haiman Kalenga (09) Mwanafunzi wa drs la kwanza shule ya msingi Livingston na Hussein Moshi (18) mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya msingi Rusimbi.

Hata hivyo kamanda Mtui amewataka wazazi na walezi kuwazuia watoto wao kuogelewa ziwani na katika mabwawa kwani si salama hasa msimu huu wa mvua ili kuepusha vifo vinavyosababishwa na maji.