Bi Domitila Muhoza (53) mkazi wa masanga Manspaa ya Kigoma Ujiji akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Maweni mkoani Kigoma baada ya kuvamia na kunusurika kukatwa ulimi. |
Akizungumza na blog hii Bi Muhoza
amesema wakati akielekea kanisani alisikia mtu akimshika kwa nyuma na kuanza
kumpiga maeneo ya usoni na kutaka kumkata ulimi huku akimuomba pesa na vitu
vingine vya thamani alivyokuwa navyo.
“Wakati akiendelea kunipiga
aliingiza mkono mdomoni ili anikati ulimi, kilichonisaidia nilimng’ata meno
ndio akanichia, licha ya kuwa alikuwa ameshaniumiza sana usoni na mdomoni na
kuniambia nimpe pesa lakini sikuwa nazo nikamuachia nguo nilizokuwa nazo”
alisema Bi Muhoza.
Aidha Bi Muhoza alisema kuwa,
hakumtutambua mtu Yule kwasababu alikuwa ameshaumia ambapo baada ya mtu Yule
kukimbia walikuja watu na kumsaidia kumpeleka hospitali ya Rufaa ya mkoa Maweni
kwaajiri ya matibabu.
Kwa upande wake Kaimu Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Maweni Daktari Fadhili kibaya, amesema
walimpokea mama huyo akiwa na hari mbaya akivuja damu mdomoni huku akiwa na
majeraha sehamu za usoni ambapo alipatiwa matibabu.
“Ulimu na sehemu zingine zenye
majeraha zilishonwa na kupewa dawa na mpaka sasa amelazwa akiuguza majeraha
yake, Pia hakuna athari kubwa aliyoipata kwenye ulimi hivyo tunategemea baada
ya muda ulimi utapona na kuanza kufanya kazi kama kawaida” alisema Daktari
Kibaya.
Nae Lovenes Lauson ambaye ni mkwe wa
Bi Muhoza alisema walipigiwa siku na kuambiwa mama yao amevamiwa na majambazi,
wakaamua kwenda eneo la tukio na kumkuta ana hali mbaya ndipo wakamchukua na
kumpeleka Polisi kwaajiri ya PF 3 na hatimaye wakampeleka Hospitali.