Watu wanaofanya shughuli ya kuchinja wanyama katika machinjio ya Ujiji mkoani Kigoma wakiendelea na shughuli hiyo kabla ya kufungwa kwa machinjio hiyo. |
Manispaa ya Kigoma ujiji imesaria na machinjio moja inayopatikana
Ujiji ambayo hata hivyo haikidhi mahitaji ya wakazi wa manispaa hiyo, hii ni
kufuatia Mamlaka ya Chakula na Dawa
Nchini -TFDA kanda ya magharibi kufunga machinjio ya kibirizi kutokana na kuwa na miundombinu mibovu
inayohatarisha afya ya binadamu.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya TFDA kupokea
malalamiko kutoka kwa wachinjaji wa
machinjio hiyo kuhusu ukosefu wa maji jambo lililomfanya Meneja wa TFDA Kanda
ya Magharibi Edgar Mahundi kufika katika eneo hilo na kujionea hali ya
miundombinu ilivyo chakavu jambo
lililomfanya kufunga machinjio hiyo.
Kwa upande wao wachinjaji na wanunuzi wa jumla
kwenda mabuchani wamesema kuwa kwa kawaida ruzuku ya serikali na ushuru wanaolipa wafanyabiashara
ungetakiwa kurekebisha machinjio hiyo lakini hakuna kinachofanyika.
“Ni jambo la ajabu serikali kushindwa kurekebisha
machinjio hiyo licha ya kuwa kila siku michango ya ushuru na kodi za wananchi
zinakusanywa sasa ka ni hivyo pesa zile zinaenda wapi?” waliuliza.
Naye mkuu wa idara ya uvuvi na mifugo manispaa ya
kigoma Ujiji dr John Shauri ameonyesha kupokea hatua hiyo kwa mshituko huku
akisisitiza kuwa tatizo ni ufinyu wa bajeti huku akibainisha kuwa tayari kuna
pesa imetengwa kwaajiri ya kuboresha
machinjio hiyo.