Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Apr 3, 2017

UDHAIFU WA UBORA WA BOTI NI CHANZO CHA AJARI ZIWA TANGANYIKA

 


Abiria wakiwa kwenye boti tayari kwa safari katika ziwa Tanganyika mkoani Kigoma
Boti za mizigo zikiwa katika bandari ndogo ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujij.
Na Emmanuel Senny
Katika Kupambana na suala la Ajari za majini, imegundulika kuwa utengenezwaji wa maboti chini ya kiwango ndio sababu ya ajari zinazoendelea kutokea katika ziwa Tanganyika.

Mkurugenzi mkuu wa SUMATRA Gilliard Ngewe amebainisha hayo hivi karibuni kwa kusema kuwa kwa muda mrefu wamefanya ukaguzi na kugundua sababu hizo lakini moja wapo ikiwa ni ubora wa vyombo hivyo.

Amesema kuwa, kwa muda mrefu sasa wanafanya ukaguzi wa vyombo hivyo na ukaguzi unaonyesha kuwa 70%  ya vyombo hivyo huwa na ubora wakati 30% vikiwa havifikii viwango vinavyotakiwa kisheria.

“Kwa nini tuwe na asilimia 30 yote hii? Kwahiyo tunataka kupunguza asilimia hizo kwa kushirikiana na mafundi wanaotengeneza vyombo hivyo ili kufikia asilimia 100 ya vyombo vyenye ubora” alisema Bw. Ngewe.

Aidha katika kutatua changamoto hiyo Bw. Ngwewe amewataka mafundi wa maboti kuungana kwa pamoja na kupeana ujuzi ambao utawafanya kujenga maboti yenye ubora unaotakiwa.

Kwa upande wao  mafundi wa vyombo hivyo ambao ukaguzi unaonyesha kuwa wao ndio chanzo cha ajari za majini kwa kutengeneza vyombo chini ya viwango akiwemo Hamisi Alimas, Juma Ibrahimu na Paulo William  wamesema  kuwa sababu ajari huletwa na utaratibu wa upakiaji wa mizigo, kama mizigo ikiwa mingi kushinda kiwanga cha kinachotakiwa kwenye boti.

“Huwa tunawashauri matajiri wanaotupa kazi ya kutengeneza vyombo hivyo kuacha kupakia mizigo mingi lakini kwasababu ya tamaA ya pesa wanakiuka na kuzidisha mizigo ambapo baadae boti huzana mara inapopata msukosuko majini” walisema.

Contact:
0765617630
email: 
sennyemmanuel@gmail.com