Wafanyabiashara na wakulima wilayani Kibondo mkoani Kigoma wameulalamikia uongozi
wa halmashauri ya wilaya hiyo kutokana na ongezeko la bei za ushuru wa bidhaa hali
inayopelekea wanunuzi kutoka nje ya wilaya
waliokuwa wakifuata mazao ikiwemo mahindi na maharage, kuacha kununua bidhaa hizo
kwa kile kinachodaiwa ni kutokana na bei za ushuru kuongezeka.
Wakizungumza
na waandishi wa habari siku chache ikiwa ni baada ya wafanyabiashara na wakulima
hao kuandamana katika ofisi za jumba la maendeleo mjini kibondo, wamesema ushuru
umepanda kutoka shilingi elfu moja mia tano hadi elf mbili na kufikia elfu sita
kwasasa bei hiyo ikiwa ni kwa mfuko wa debe sita hali ambayo imewafanya wauze bidhaa
hizo kwa mda mrefu tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Wamesema
licha ya kutumia jitiahada zao za kujikwamua kimaisha kupitia biasharana na kilimo,
hali ya mzunguko wa fedh aimekuwa ngumu kutokana na kitendo cha halimashauri hiyo
kupandisha bei za ushuru wa mazao.
Kwaupande
wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya kibondo Bw. Seif Salum
amesema kiwango cha bei ya ushuru kilichopangwa hakizidi aslimia tano ya bei za
mazao, na kuwataka wafanyabiashara kuzingatia kanuni na sheria zinazokuwa zimepangwa
na halmashauri kwa kuzingatia msimu wa upatikanaji wa bidhaa za kilimo.
“Cha
msingi ni kuzingatia tu mana mabadiriko yaliyofanyika si kwa lengo la kuwakomoa
au kujinufaisha bali kwa lengo la kuinufaisha halmashauri pamoja kuangalia
ugumu wa upatikanaji wa bidhaa husika” amesema.