Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Apr 26, 2017

PICHA: Covenant Bank yajidhatiti kuboresha maisha ya Mama Lishe nchini



Benki ya Covenant Bank imetoa mafunzo kwa ambapo licha ya kutoa elimu pia itawawezesha Mama lishe wote nchini kwa kuwaunganisha na huduma za bima ya matibabu na bima ya mazishi, huku wakiwezeshwa kutumia huduma za benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja akifafanua jambo kwa mam lishe mbalimbali wa Dar es Salaam wakati wa semina ya mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Benki hiyo itawawezesha Mama lishe wote nchini kwa kuwaunganisha na huduma za bima ya matibabu na bima ya mazishi, huku wakiwezeshwa kutumia huduma za benki hiyo. Huduma hizo zinatotela kwa kushirikiana na Taasisi ya Basila Mwanukuzi.

Mama lishe wakiwa wanasikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa benki, ( Hawapo pichani)

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja (Katikati) akisisitiza jambo kwa Kiongozi wa mama Lishe jijini Dar es Salaam, Getruda Kweka wakati akizungumza na waandishi wa habari, Benki hiyo itawawezesha Mama lishe wote nchini kwa kuwaunganisha na huduma za bima ya matibabu na bima ya mazishi, huku wakiwezeshwa kutumia huduma za benki hiyo. Kulia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi.