Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jul 21, 2015

LIVERPOOL WAMNASA BENTEKE

Klabu ya Liverpool nchini Uingereza imefanikiwa kumsajiri mshambuliaji wa Klabu ya Aston Villa Christian Benteke kwa kitita cha pauni milioni 32.5.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 12 katika mechi 12 katika msimu wa mwaka 2014-2015 na kuisadia Villa kusalia katika ligi kuu ya Uingereza.

Liverpool imekubali kutoa kitita hicho baada ya kupokea kitita cha pauni milioni 49 kutokana na mauzo ya mchezaji Raheem Sterling aliyehamia Mancity.

Benteke aliyekuwa amesalia na kandarasi ya miaka 2 katika klabu ya Villa anaungana na wachezaji waliosajiliwa na Liverpool msimu huu ili kukiongezea nguvu kikosi cha Brendan Rodgers.

Ukiachana na Benteke wachezaji waliosajiliwa na Liverpool mpaka sasa ni Dan Ings, Divok Orig aliyekuwa kwa mkopo lile, James Milner, Joe Gomez, Roberto Filminho, Bogan, Natahiel Clyine 

Benteke anatarajiwa kuziba pengo la Mshambuliaji wa Uingereza aliyemajeruhi Daniel Sturridge, Sturridgealiichezea timu hiyo mara 18 msimu uliopita kutokana na msururu wa majeraha na atasalia nje hadi mwezi Septemba akiuguza jeraha la kiuno.