AJARI
ya moto imetokea mkoani Kigoma na kuteketeza Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya
Kibondo huku chanzo chake kikiwa bado hakijajulikana.
Wakizungumza
na Tanzania Daima mashuhuda wa tukio hilo ambao ni walinzi wa ofisi hizo, Ndaimisi
Gwakila alisema kuwa, tukio hilo lilitokea mida ya saa 7 kasoro usiku wakati
wakikagua usalama wa ofisi hizo.
Alisema
kuwa, wakati wakiendelea na ukaguzi wakaona moto unawaka kwenye paa ya jingo hilo ikabidi waombe msaada
kwa Polisi waliokuwa wakilinda Benk ya CRDB jirani na ofisi hizo ndio wakafanya
taratibu za kuzima moto ule.
“Kwa
kushirikiana na Polisi wale ilibidi tutoe taarifa Kituo cha Polisi, Polisi
walikuja na ila maji yalikuwa ni tatizo.
“Wananchi
wa maeneo haya na viongozi waliopata taarifa walijitahidi kushirikiana kuzima
moto lakini ilishindikana ikabidi waanze kubomoa sehemu ambazo moto ulikuwa
hauwaki sana na kutoa vitu” aliserma Gwakila.
Nae
Kamanda wa Polisi Wilayani humo, Marco Joshua alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kusema kuwa, kilichofanya washindwe kuzima moto ule baada ya kupata
taarifa ni kutokana na kutokuwepo kwa kikosi cha zimamoto kwani kama kikosi
hicho kingekuwepo ingekuwa rahisi kuzima moto ule.
“Kinachofanya
kikosi hicho kisiwepo ni kutokana na tangu nishati ya umeme kuingia wilayani
hapo hakujawahi kutokea janga kama hilo ila kwasasa inabidi serikali iangalie
suala ya kuweka kikosi cha zimo Kibondo” alisema Joshua
Kamanda
Joshua aliongeza kuwa, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ila wanaendelea
kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.
Kwa
upende wake Mkurugenzi wa Maendelea ya Halmashauri hiyo, Juda Fabrious, alisema
kuwa moto hupo uliteketeza ofisi za masijara ya wazi na ya siri, ofisi ya
utumisi pamoja na Ofisi yake Mkurugenzi.
“Vitu
vyote vilivyokuwemo ndani ya ofisi hizo viliteketea hivyo tunasubiri watu wa
kufanya tathimini waje ili kujua gharama ya vitu vilivyoteketea” alisema
Fabrious.