Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jul 16, 2015

MAMBO 10 USIYOJUA KUHUSU RAIS DR. JAKAYA KIKWETE

Akiwa amebakiza miezi michache kutoka madarakani leo tunakuletea mambo 10 usiyoyajua kuhusu Rais Jakaya Kikwete.

1. Rais kikwete anatoka kwenye familia ya watoto tisa huku na yeye akiwa na watoto tisa
Pia yeye ni mtoto wa sita katika familia yao.
Rais alizaliwa tarehe 7th oktoba 1950,baba yake ni mzee Halfani Mrisho Kikwete na mama yake ni Asha Jakaya Kikwete wote wakiwa ni wazaliwa wa kijiji cha Msonga mkoani Pwani.
2. Rais Kikwete ana shahada ya uchumi
ambayo aliipata kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.

3. Rais alikuwa ni mmojawapo wa watumishi wa jeshi la wananchi
na alipata mafunzo  hayo ya kijeshi mwaka 1972 hadi mwaka 1976.

4. Rais Kikwete alichaguliwa kuwa waziri akiwa na umri wa miaka 44 na kuweka historia  ya kuwa waziri mwenye umri mdogo kuwahi kuitumikia serikali kuu.
Rais Kikwete baada ya kuitumikia serikali kuu kwa miaka sita aliteuliwa kuwa waziri wa fedha ambapo aliweza kuitumikia nafasi hiyo kwa mafanikio makubwa.

5. Rais Kikwete alitumikia nafasi ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa miaka kumi.
Pia aliweka historia ya kuwa waziri wa kwanza hapa nchini kukaa madarakani kwa kipindi kirefu.

6. Rais Kikwete si mbaguzi wa dini
Kwa baadhi ya viongozi wa Afrika,Rais Kikwete ni mmojawapo wa viongozi ambao ni wavumilivu sana linapokuja suala la dini.
Rais yeye ni muumini wa dini ya kiislamu lakini uwa anajichanganya na wakristo pia aliwahi kupewa zawadi ya biblia.

7. Rais Kikwete alifuta baadhi ya madeni ya wawekezaji kipindi cha utawala wake
Chini ya uongozi wa Rais Kikwete Tanzania imeweza kukua kiuchumi na kupanua uwekezaji kwa kiwango kikubwa kutokana na misamaha ya kodi.

8. Rais Kikwete ni rafiki wa mtandao wa Twitter
Rais  ni maarufu sana katika mitandao ya kijamii hasa kwenye ukurasa wa twitter kutokana na kujiweka karibu na wananchi pamoja na marafiki zake kupitia mitandao.

9. Rais Kikwete ni mpenzi wa mpira wa kikapu
Rais ni mmoja wa wapenzi wa michezo hasa mpira wa kikapu.
Kipindi akiwa bado anasoma alishiriki mashindano mengi ya mpira wa kikapu pia alikuwa kiongozi mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu kwa miaka 10.

10. Rais Kikwete haweki madaraka yake mbele
Jakaya ameitumikia Tanzania kama Raisi kwa mihula miwili na ameridhika na utawala wake haitaji tena kukaa madarakani, katika moja ya hotuba zake alisema kwamba “ifikapo mwezi wa kumi mwaka huu nitapumzika maana nimekuwa na wakati mgumu kwa miaka mingi kwenye uongozi wangu.”