Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jul 16, 2015

SUNDAY OLISEH ATEULIWA KUWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Sunday Oliseh,40 ametangazwa na Shirikisho la Soka la Nigeria NFF kuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria kwa mkataba wa miaka 3.

NFF imemchagua nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wa timu hiyo Stephen Kesh.

Akizungumzia nafasi hiyo baada ya kuteuliwa kuwa kocha wa timu hiyo ya taifa, Sunday Oliseh amesema Nigeria ni nchi yenye vipaji vingi nani wakati wa kurudisha heshima waliyokuwanayo katika mpira wa miguu.

Oliseh ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu za Borussia Dortmund, Ajax na Juventus amesema kazi ameyopewa ni kubwa katika soka la Afrika na ili kufanikisha hilo anahitaji sapoti kutoka kwa kila mtu.

Ameongeza kuwa kazi ameyopewa na NFF ni kubwa naya heshima kwake na hivyo anatarajia kufanya kazi nzuri kwa kushirikiana na wanaijeria wote kuweza kupeperusha bendera ya nchi hiyo na kazi inaanza sasa sio kuanza kusubiri.

Kwa upande wa NFF kupitia kwa rais wa chama hicho, Amaju Pinnick amesema Oliseh ni mtu bora na amekuwa na mchango mkubwa kwa soka la Nigeria kwa kutoa ushauri kwao na kufanya nao kazi kuhakikisha soka la Nigeria.

Nae Katibu Mkuu wa NFF, Dr. Mohammed Sanusi amesema kwa sasa timu ya taifa ina michezo muhimu ndani ya wiki kadhaa mbele na hivyo wanatakiwa kuanza maandalizi mara moja.

Sunday Oliseh aliichezea timu ya taifa ya Nigeria michezo 63 na kuisaidia kushinda ubingwa wa Afrika 1994 na kushinda medali ya dhahabu ya michezo ya Olympic ya mwaka 1996, na pia ni mchezaji wa 4 kutoka kikosi cha Super Eagles cha 1994 kufundisha timu ya taifa baada ya Austin Eguavoen, Samson Siasia na Stephen Kesh.