WAKAZI
wa Manispaa ya Kigoma Ujiji
wameiulalamikia uongozi wa Halmashauri kwa kushindwa kupambana na hari ya
uchafu inayoikabili Manispaa hiyo kutokana na kuenea kwa uchafu katika maeneo
ya watu.
Katika
Manispaa ya Kigoma-Ujiji suala la usafi linaonekana kushindikana kutokana na
uchafu unaozalishwa kila siku kutokusanywa na kupelekwa sehemu husika kwa muda
muafaka na kusababisha uchafu kuzagaa hovyo licha ya wananchi kulalamikia suala
hilo kila siku.
Wakizungumza
na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti, wakazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji
walitoa malalamiko yao kuhusu hali ya uchafu katika manispaa hiyo.
Dampo la uchafu lililoko maeneo ya Mwanga Center ambalo ni moja ya dampo linalolalamikiwa kutokutolewa kwa uchafu. |
Festo
Yothamu ambaye ni mfanyabiashara wa vyuma chakavu eneo la Mwanga Centre alisema
kuwa, wanapata kero ya harufu mbaya pia
muonekano wa uchafu kutokana na dampo la
uchafu lililoko maeneo yao ambalo hujaa kwa muda mrefu bila kuondolewa.
Alisema
kuwa, dampo hilo linaathiri ya kutokuzolewa uchafu kwa muda muafaka kama
yalivyo madampo ya maeneo mengine nakusababisha uchafu kuingia mpaka barabarani
na kusogea karibia na maeneo ya kazi za watu huku harufu mbaya ikiendelea kuwa
kero kwa watu kila siku.
Yotham
aliongeza kuwa, kuwa hari hii ya uchafu
inaweza kupelekea mlipuko wa magonjwa hivyo serikali ambao ndio wana dhamana ya
kuangalia usafi wa Manispaa waangalie ni wapi wanakosea ili kurekebisha tatizo
hili.
Dampo la uchafu lililoko maeneo ya Mwanga Center ambalo ni moja ya dampo linalolalamikiwa kutokutolewa kwa uchafu. |
Aidha
Aisha Issa ambaye ni Mama Ntilie eneo la Mwanga Centre alisema kuwa dampo
lililopo maeneo hayo limekuwa kero kubwa kwa biashara yake hasa kipindi harufu
inapokuwa kali husababisha wateja kutokula chakula
Alisema
kuwa wanajitahidi kutoa ushirikiano kwa serikali za mitaa ambazo zinasimamia
zoezi la kukusanya uchafu kwenye makazi ya watu kwa kuchangia shilingi 1000/=
ila bado serikali haijari kuondoa uchafu unaokusanywa katika dampo hilo.
“Hakuna
mtu anayependa kula chakula sehemu nambayo inaharufu mbaya, sasa hapo ndio sisi
wauza chakula tunakosa wateja kabisa’ alisema Issa.
Nae
Abdara Kimenya ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kisangani, alizungumzia zoezi la
uzoaji wa taka majumbania kuwa zoezi hilo linaonekana kukwama kutokana na changamoto ya kutokuwepo kwa vitendea kazi kama matololi na mapipa ya
kuhifadhia taka kabla hazijachukuliwa..
“Gari
zinatakiwa kuwa Zaidi ya mbili pia serikali inatakiwa kugawa katika mitaa
mapipa ya kuhifadhi uchafu kabla haujakusanywa, hata kama pipa moja likitumika
kwa nyumba hata 10 ili kukomesha uchafu kuzagaa” alisema Kimenya.
Kwa
upande wake Afisa Afya wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji Leonida Mbwiliza, alisema kuwa
suala la uchafu katika Manispaa lipo ila jitihada zinafanyika ili kupambana na
suala la uchafu ambapo serikali za mitaa zinaendesha zoezi la kukusanya taka
majumbani na kuzipeleka kwenye madampo.
Alisema
kuwa changamoto zinazochangia kuwepo kwa uchafu ni kukosa vitendea kazi
kutokana na Manispaa kuwa na gari mbili mabazo bado hazitoshi pia Mitaani vifaa
vinahitajika ili kuwawezesha wakusanyaji wa uchafu majumbani kufanya kazi
vizuri na kwa muda muafaka.
“Gari
zilizopo kwanza ni za kizamani pia ni madogo, Gari moja linabeba tani tatu
hivyo huzoa takataka kidogo wakati taka zinazozaliishwa ni nyingi, ukweli
magari haya yameshachoka leo zima kesho bovu sasa huwezi kutegemea magari hayo”
alisema Mbwiliza.