Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jul 16, 2015

UMEME WA REA KUWASHWA MWEZI SEPTEMBA

Vijiji vya Halmshauri ya Kigoma Vijijini na Uvinza  za mkoa wa Kigoma zinatarajiwa kuwashiwa umeme wa REA mwezi septemba.

Akizungumza na Kigoma Online News, Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Kigoma, Bw. Michael Kidoto amesema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho nabaada ya hapo watawasha.

Kidoto amesema kuwa kwa sasa wanaunganisha waya kutoka eneo la Mwandiga hadi kilipo kituo cha kusambazia umeme (Power Station).

Nae Injia wa REA, Godfrey Josephat amewatoa hofu wananchi wa vijiji ambavyo umeme haujafika.

Godfrey amesema kwa sasa wapo katika awamu ya pili na wanapeleka umeme katika vijiji ambavyo serikali imevipitisha kupelekewa umeme.

Amesema vijiji ambavyo havijapelekewa umeme visubiri awamu ya tatu ambayo mchakato wake utaanza mara moja baada ya awamu ya pili kukamilika.

Aidha Injinia Josephat amesema kijiji cha Kagunga hawataweza kukipelekea umeme hata katika awamu ya tatu kutokana na kutokuwepo miundombinu kufika kijijini hapo na tayari wamewasiliana na Wizara ili iwasiliane na wenzao wa Burundi ili waweze kupata umeme kutoka Burundi kutokana na Kijiji hicho kuwa karibu zaidi na nchi hiyo.