Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Nov 27, 2015

ASKARI POLISI WATATU KIGOMA WAFUKUZWA KAZI KISA MITANDAO YA KIJAMII


JESHI La Polisi mkoani Kigoma limethibistisha kuwafukuzwa  kazi askari wake watatu  akiwemo Johnson, Pisii Justine na Mesi ambaye ni askari wa kike kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

Tarifa hiyo ilitolewa hapo jana na Kamanda wa Polisi mkoani hapa Ferdinand Mtui ambapo alisema Askali hao wali fanya tukio hilo Augost mwaka huu na baada ya kubainika taratibu za kuwashitaki zilifanyika ambapo ilipofika Novemba 12 mashitaka yao yalifika mwishoni ambapo kutokana na ukubwa wa kosa walilofanya ikamuliwa wafukuzwe kazi.

Kamanda Mtui alisema kuwa, walipofukuzwa kazi walipewa haki ya kukata rufaa na walikata rufaa kuhusu tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui akizungumzia tukio la Askari wake watatu kufukuzwa kazi kwasababu ya kueneza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii.