MTU
mmoja ajulikanaye kwa jina la Gerevasi Kassiano(25) ambaye ni dreva bodaboda
mkazi wa Burega amefariki dunia baada ya kugongwa na gari linalotumiwa na
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Ferdinand Mtui.
Akizungumzia
tukio hilo Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Masud Kalembe ambaye ni shuhuda wa
tukio hilo alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Desemba 26 mwaka huu majira ya
saa 8.30 mchana eneo la Lubengera katika Manispaa ya kigoma Ujiji ambapo gari aina ya Landcruser yenye vioo vyeusi (tinted) linalotumiwa na RPC
lilimgonga kijana huyo na kufa papo hapo.
Alisema
kuwa, gari hilo lilikuwa likitokea barabara ya Kigoma Ujiji kwenda kigoma
mjini, na baada ya dreva wa gari hilo kuyapita kwa pamoja magari mawili ya
abiria (Hiace) yaliyokuwa yakifuatana akajikuta
akigongana uso kwa uso na dereva wa bodaboda na kufa hapohapo.
“Maiti
ilitolewa chini ya gari la RPC, na kitendo hicho kilipelekea baadhi
ya madereva wa bodaboda kituo cha Lubengera kufunga njia wakitaka haki itendeke ndipo askari waliovaa kiraia
waliokuwa katika gari la defender walipiga bomu moja la machozi ili
kuwatawanya raia, hapo hapo vijana wawili walikamatwa na kutupwa mahabusu huku
pikipiki tatu zikishikiliwa na jeshi hilo.
“Ili
kuinusuru serikali ya awamu ya tano isionekane ya kufumbia macho matukio yoyote
yale, sikuwa na budi kuwafuatilia vijana hao hadi wakatolewa kwa ushirikiano wa
Mkuu wa wilaya Saveli Mwangasame, ila nachojiuliza kwa nini baadhi ya askari
wanajawa na vibuli vya magwanda tu wakati Watanzania wote tuha haki sawa”
alisema Kalembe.
Adha baadhi
ya waendesha bodaboda kituo cha Maweni na Lubengela wakiomba hifadhi ya majina
kwa usalama wao katika shughuli zao, kwa nyakati tofauti walikiri kutokea kwa
tukio lilomuua mwenzao.
Nae
Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa Maweni, Fadhili Kibaya, alikiri kupokea maiti ya kijana aliyegongwa na gari mida ya
saa 9:00 alasiri na maiti kuhifadhiwa chumba cha mochwari kwa ajili ya taratibu
zingine.
Kwa
upande wa Kamanda wa Polisi mkoani
Kigoma, SACP Fernand Mtui,
alipohojiwa kwa njia ya simu juu ya tuko hilohilo alijibu kuwa “Ni kweli ila
ajari hiyo ni kama ajari zingine, ndugu wakitaka maelezo kamili waje kituoni
watapewa namna ilivyokuwa”.
Hata
hivyo leo hii Desemba 27 asubuhi ya saa 4 zilionekana gari mbili eneo la tukio
na kuona shughuli ya upimaji wa ajali ikifanyika chini ya ulinzi mkali, hali
inayowashangaza raia kwa jeshi hilo kushindwa kuwajibika pale wanapokosea wao.