Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 27, 2015

ARSENAL APIGWA 4-0 YASHINDWA KUONGOZA LIGI

Klabu ya Arsenal imeshindwa kuongoza ligi kuu nchini England baada ya kufungwa mabao 4-0 na Southampton katika mchezo uliopigwa jana usiku katika dimba la St Mary.

Mabao kutoka kwa Cuco Martina, Shane Long (2) na Jose Fonte yaliisaidia Southampton kupata point tatu muhimu mbele ya The Gurnners ambao awali walitarajiwa wangeshinda mchezo huo.
Mchezaji wa Southamptoni Shane Long aliyefunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Arsenal.

Arsenal ilikuwa na nafasi ya kuongoza ligi kama ingeshinda kutokana na timu ya Leicester ambayo inaongoza ligi hiyo kufungwa na Liverpool bao 1-0 hapo jana.

Kwa upande wa Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger  alishindwa kuendeleza ubabe wake baada ya wiki iliyopita kuifunga anchester City siku ya Jumatatu, lakini walipofika kwa Southampton hawakufua dafu na kukubali kipigo hicho cha mabao 4-0.





Matokeo yote Mechi za jana.

Sat 26 Dec 2015 - Premier League