Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majariwa ameiagiza mamlaka ya bandari mkoani Kigoma (TPA)
kupitia upya zoezi linalolalamikiwa na wananchi kuhusu fidia zao.
Wananchi wa Kata ya kibirizi mkoani Kigoma wakiwa na mabango yaliyolenga kumpa ujumbe Waziri Mkuu Kassim Majariwa kuhusu fidia za upanuzi wa bandari na ujenzi wa bandari ya nchi kavu Katosho. |
Alisema kuwa, kisheria wananchi wote wanaohamishwa katika maeneo Yao hutakiwa kulipwa fidia ambapo katika mradi wa upanuzi wa bandari ya Kigoma ambao ulipeleka kuhamishwa kwa baadhi ya wananchi wa kibirizi, wapo waliolipwa fidia na wengine hawakulipwa huku wengine wakilalamikia kulipwa fidia ndogo.
"Nimeona wananchi wakiwa na mabango
wakinihitaji niwasaidi katika suala la fidia na wanadai haki haikutendeka pia
hata Mbunge wao Zitto Kabwe ameligusia malalamiko ya wananchi " alisema
Waziri Majariwa.
Aidha Majariwa alisema kuwa, Mamlaka ya
bandari inatakiwa kupitia upya suala la fidia kwa wananchi wa kibirizi kwa
kukagua kila eneo la mtu na thamani ya pesa aliyolipwa pia kuwalipa wale ambao
hawakulipwa.
Wananchi wa Kata ya kibirizi mkoani Kigoma wakiwa na mabango yaliyolenga kumpa ujumbe Waziri Mkuu Kassim Majariwa kuhusu fidia za upanuzi wa bandari na ujenzi wa bandari ya nchi kavu Katosho. |
"Suala la hili litafanyika mara
moja mara baada ya mimi kuonana na viongozi wa mamlaka ya bandari na nitahitaji
kama kuna mtu alilipwa fidia ndogo basi aongezwe kulingana na thamani ya eneo
lake na kwa wale ambao hawajalipwa kama maeneo Yao yako kwenye mradi basi
walipwe mara moja " alisisitiza Waziri Majaliwa.
Hata hivyo Waziri Majaliwa alisema kuwa,
suala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni endeleavu ambapo kwa kigoma kuna
mradi wa upanuzi wa bandari na ujenzi wa bandari ya nchi kavu na miradi hii
yote inagusa maeneo ya wananchi hivyo serikali inatakiwa kulipa fidia stahiki
kwa kila mwananchi wa eneo husika.
Awali Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto
Kabwe, alimtaka Waziri Majaliwa kusikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu suala
la fidia ambalo linaonekana Kuwa kero kutokana na wengi kulipwa fidia ndogo
huku wengine kutokulipwa kabisa.