Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, amewataka
wakimbizi wanaokuja nchini ili kuomba hifadhi kuacha kubeba siraha nakujanazo
nchini kwani kwa kufanya hivyo kunachochea vitendo vya kiharifu.
Akizungumza
na wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma hapo
jana, Waziri Mkuu alisema kuwa, kumekuwa na vitendo vingi vya ujambazi wa
kutumia sirahamkoani hapa ambapo utafiti unaonyesha matukio mengi hufanywa na
raia wa kigeni.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. |
Alisema
kuwa, kwakuwa wakimbizi wote wako nchini ili kuokoa maisha yao kutokana na
machafuko nchini kwao hawana budi kufuata sheria na taratibu za nchi ya
Tanzania ili waipate ile amani waliyoifuata.
“Sawa
tumewapokea na kuwapa hifadhi ila jambo la msingi ambalo hamtakiwi kulifanya ni
kuja na siraha ya aina yoyote kambini, kama mtu anataka kuja nchi na ana siraha
ni vyema aiache huko badala ya kuja nayo na kumletea madhara” alisema Waziri
Majaliwa.
Aidha
Waziri Majaliwa, aliwataka wakimbizi wote walio na siraha wazisalimishe ili
kambi ziwe na usalama badala ya kusubiri mtu kukamatwa na siraha jambo ambalo
litamuweka matatani.
Baadhi ya wakimbizi kutoka Burundi na Congo waishio katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassimi Majaliwa (hayupo pichani) wakati akiwahutubia. |
“Kama
kuna mtu umeficha siraha mahari popote ni vyema ukatumia busara kwa kwenda
kuichukua na kuikabizi kwa Jeshi la Polisi badala ya kusubiri mpaka tukukamate,
na tukikukamata lazima uchukuliwe hatua mana hatutaki kuhifadhi majambazi bali
tunahifadhi raia wema.
“Suala la usalama ni la muhimu kwa kila
mkimbizi pia ni muhimu kwa majirani ambao ni watanzania sambamba na watoa huduma
kambini humo, hivyo ni vyema kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake ili siku mkirudi
nchini kwanu mrudi mkiwa salama” alisisitiza Waziri Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majariwa, akiangalia ngoma za jadi zilizokuwa zikichezwa na Wakimbizi raia wa Burundi katika kambi ya Nyarugusu. |
Akitoa
maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu, Sospeter Boyo,
alisema kuwa, kambi hivyo ilifunguliwa Novemba 1996 kwa lengo la kuhifadhi
wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kocngo waliokuwa wakikimbia vita
vya wenyewe kwa wenyewe nchini kwao.
Alisema
kuwa, kambi hiyo yenye ukubwa wa kilometa za mraba 28, ina uwezo wa kuhifadhi
wakimbizi 50,000 lakini kwasasa ina wakimbizi 151,032 ambao ni mara tatu ya
zaidi ya uwezo harisi wa kambi hiyo.
Boyo
aliongeza kuwa, tangu Aprili mwaka huu, idadi ya wakimbizi iliongezeka hadi
kufikia 151,032 ambapo miongoni mwao ni Wakongo 61,313, Warundi 89,619,
Wanyarwanda 75, Waganda 12, Wasudan Kusini wane, Wakenya wane, Msomali mmoja,
Mzimbabwe mmoja na Mwaivory Cost mmoja.