Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk. Leonard Subi. |
Akizungumza
na blog hii, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ukumbi Kata ya Machinjioni, Jumanne Baheza,
amesema, mvua hiyo ilinyesha jana majira ya saa 5:00 asubuhi na kusababisha
kaya mbili kubomoka huku vyoo 15 vikisombwa na mafuriko.
Amesema,
kusombwa kwa vyoo hivyo kulisababisha kaya 15 kukosa vyoo huku kukiwa na hofu
ya kutanda kwa magonjwa ya mlipuko kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na uchafu
wa vyoo kupelekwa kwenye vyanzo vya maji ambayo wakazi wa eneo hilo huyatumia.
“Sasa
kuna uwezekano mkubwa wa wananchi kupata magonjwa mana kila siku hutumia maji
yanayotoka kwenye vyanzo vya maji (bondeni) ambako ndiko uchafu wa vyoo
ulielekea huko,” amesema Baheza.
Awali
katika kikao cha Mkoa kilichoketi Novemba 2015 kilichoadhimia kudhibiti hari ya uchafu katika mkoa huu,
Mganga Mkuu wa Kigoma Leonard Subi, alisema kuwa Kigoma inakabiliwa na ukosefu
wa vyoo bora kwa asilimia 25 na vyoo
vingi vimejaa.
Aidha
takwimu hiyo ya Mganga mkuu inaonyesha kuwa tatizo la ukosefu wa vyoo
linaongezeka kutokana na athali za mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa na
kupelekea hofu ya magonjwa ya mlipuko.
Hata
hivyo Baheza amewataka wakazi wa kata ya Machinjioni kufuata sheria na taratibu
za afya ikiwa ni kunawa mikono kwa sababuni kabla na baada ya kula sambamba na
kunywa maji yaliyochemshwa pamoja na
kuacha tabia ya kuoga kwenye vyazo vya maji kama alivyoagiza Mganga wa Mkoa.