Watu wawili wakazi wa Kata ya Kagunga kitongoji cha Zashe Mwambao wa Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji kutokana na kunyesha mvua kubwa huku kaya tisa zimekosa makazi ya kuishi ikiwemo nyumba mbili kuangukiwa na kifusi cha mlima.
Akizungumza
na blog hili baada ya kuulizwa kuhusu tukio hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya
Kigoma, Joshua Elisha alisema kuwa, tukio hilo lilisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha
Januari 22 ambapo sehemu mbalimbali mkoani hapa ziliathiliwa na mvua ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya
madaraja pamoja na makazi ya watu.
Alisema
kuwa, waliokufa katika tukio hilo ni watu wawili ambao walijulikana kwa jina moja moja akiwemo Kizigo
(45) na Malisela (70) ila awali majina, umri na jinsia zao hazikufahamika.
“Nyumba
zilizoanguka ni zaidi ya sita ikiwemo nyumba waliyokuwemo marehemu ambayo
ilisombwa na maji na kusababisha vifo vyao” alisema Elisha.
Baadhi
ya wakazi wa kata ya Kagunga akiwemo Nassoro Mussa ambaye ni mgambo alisema kuwa,
mnamo Januari 22, mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku mvua kubwa ilianza kunyesha
hadi kuamkia Januari 23, ambapo maji yalikuwa mengi na kusababisha mafuriko na
kupelekea nyumba tisa kuanguka huku nyumba mbili zilizojengwa karibu na mlima
zikiangukiwa na mlima huo.
“Hadi
leo tunavyozungumza zaidi ya nyumba tisa zimebomoka na wahanga wanaishi kwa
majirani huku mali za wakazi wa kijiji hiki zikipotea baada ya kusombwa na maji
zikiwemo mashine sita za kuchakata
mafuta ya mawese” alisema Mussa.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui alithibitisha
kutokea kwa vifo vya watu hao wawili baada ya nyumba waliyokuwemo kusombwa na
maji ya mvua.
Aidha
kunyesha kwa mvua hiyo kulisababisha miundombinu mkoani hapa kuharibika ikiwemo
mradi wa chanzo cha maji kilichokasimiwa na Shirika la UN kwa lengo la
kukabiliana na changamoto ya ugonjwa wa kipindupindu katika kata ya Kagunga.
Miundombinu mingine iliyoharibika ni
pamoja na madaraja yaliyoko katika mfereji unaopitisha maji kuelekea ziwa
Tanganyika katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji ambapo serikali ya mkoa ililazimika
kufunga barabara ya Kaya Road ambayo
daraja la kwa Jaffer liliathiliwa na mvua hiyo.