Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Jan 13, 2016

KIKOSI CHA ZIMAMOTO KUKAGUA VIFAA VYA MUZIMIA MOTO KIGOMA



Jeshi la polisi kitengo cha zimamoto na uokozi mkoani Kigoma linatarajia kuanza operation ya kukagua vizima moto katika majengo mbalimbali muda wowote kuanzia sasa ili kudhibiti matukio ya moto yanayoweza kujitokeza majumbani na katika maeneo mbalimbali.

Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokozi mkoani Kigoma Kamishina msaidizi Baraza Mvano amesema katika kuzuia na kupambana na matukio ya utoakeaji wa moto jeshi hilo linatarajia kufanya operation itakayokoma mwezi February mwaka huu huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano .

Nao baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Mwanga wameomba kuwekewa vifaa hivyo na kwamba iwapo ikitokea moto katika maeneo hayo hakuna namna ya kupona zaidi ya kupata maafa na kupata hasara kwa bidhaa zao kutokana na miundombinu kutokuwa rafiki katika uzimaji wa moto.

Kwa upande wa Diwani wa kata ya Kigoma mjini Bw. Hussein Kariyango amesema bado kuna changamoto kubwa katika suala zima la uwepo wa vizima moto maeneo mbalimbali na kwamba watahahakikisha wanaisukuma manisipaa kuimarisha miundombinu ya kujikinga na moto pale unapotokea.