Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

May 8, 2016

MTOTO AFARIKI BAADA YA KUDUMBUKIA CHOONI MWINGINE MAJERUHI



Picha haihusiani na tukio.

Mtoto mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya kudumbukia choon katika  kata ya mlole Manispaa ya kigoma ujiji.


Wakizungumza na Blog hii baada ya tukio hilo, bw kasimu rusendela ambaye ni mzazi wa watoto hao pamoja na  rusendela kasimu  ambaye ni kaka yao wamesema, chanzo cha tatizo hilo ni ujenzi mbovu hali ambayo imepelekea choo kutitia na kusababisha tatizo la maafa kwa mtoto huyo.



Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi Hospital ya  Baptist Felician Kachinde amesema, wamefikishwa Hospital na kupatiwa matibabu ambapo  mauwa kasimu hali yake inaendelea vizuri lakini kaemba kasimu amefariki wakati akipatiwa matibabu.



Aidha daktary felician  amesema  kukosekana kwa kifaa cha Ventreta katika hosipital hiyo kumechangia  mtoto huyo kufariki dunia na ameitaka jamii kujenga vyoo vyenye uimara ili kuepuka matatizo kama hayo.



Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoani hapa,  SACP Ferdinand Mtui  amesema, hajapata taarifa za tukio hilo lakini zinaweza kuwa za ukweli.