Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

May 8, 2016

MWANAMKE AJINYONGA KIGOMA


Picha haihusiani na Tukio

Mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Victoria Wiso ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Buzebazeba na mkazi wa Katubuka katika Manispaa ya Kigoma Ujiji  amekutwa amejinyonga mpaka kufa kwa kutumia kamba akiwa jikoni kwake.

Akizungumza na Waandishi wa habari wiki hii, Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, SACP Ferdinand Mtui amesema, Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumatano ya Wiki hii ambapo marehemu aliamka usiku na kumfungia mme wake chumbani nae akaelekea jikoni na kutekeleza azima yake ya kujinyonga.

Aidha Kamanda Mtui amesema, Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha mama huyo kujinyonga kutokana na kutokuwepo taarifa yoyote aliyoiacha kwa maandishi.

Kwa upande wao mashuhuda wa tukio hilo ambao ni majirani wa marehemu akiwemo Zainabu Hamisi na Norata Sungura kwa nyakati tofauti wameelezea tukio hilo kuwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa mashuhuda hao, tukio hilo limeonekana kuwashangaza na kuleta hari ya sitofahamu kutokana na marehemu na mme wake kutokuwa na ugomvi wa aina yoyote ambao ungeweza kupelekea mama huyo  kujinyonga.