Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 27, 2015

LIVERPOOL YAIPUNGUZA KASI LEICESTER, MAN UTD YAPIGWA TENA, CHELSEA YADODA

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester na kupunguza kasi ya timu hiyo iliyoko kkileleni mwa Ligi ya Uingereza.

Leicester walikuwa wameenda mechi tisa bila kushindwa ligini na leo imekuwa mara yao ya kwanza kumaliza bila kufunga bao ligini msimu huu.
Mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke akishangilia bao aliloifungia timu yake, kulia ni Adam Lalana na Kushoto ni Jordan Henderson, Liverpool ilishinda bao 1-0 dhidi ya Leicester.
 Uwanjani Britannia, masaibu ya meneja Louis Van Gaal yamezidi baada ya Red Devils kucharazwa 2-0 na Stoke City. Meneja huyo amekabiliwa na shinikizo baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.

Tottenham Hotspur nao wamefufua juhudi zao za kupigania taji la ligi kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Norwich City, wakisaidiwa sana na kipa Hugo Lloris anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.

Na uwanjani Stamford Bridge, hakukuwa na habari njema sana kwa kaimu meneja Guus Hiddink baada ya vijana wake wa Chelsea kutoka sare ya 2-2 na Watford.
Kocha wa Manchester United akiondoka uwanjani kichwa chini baada ya timu yake kufungwa bao 2-0 na Stoke City.
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, aliyewafungia mabao yote mawili pia ameonyesha kadi ya manjano, hii ikiwa na maana kwamba hataweza kuwachezea dhidi ya Manchester United Jumatatu 28 Desemba.

Kiungo wao wa kati Oscar alipoteza nafasi nzuri ya kuwaweka kifua mbele alipoonekana kuteleza na kupoteza mkwaju wa penalti dakika za mwisho za mechi.

Kwa Manchester City uwanjani Etihad, ilikuwa siku ya mavuno, klabu hiyo ikipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Sunderland licha ya Wilfried Bony kupoteza mkwaju wa penalti.
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa akijilaumu baada ya kukosa goli