Kigoma Online News

FURNITURE

KALIHAMWE STATIONARY

KALIHAMWE STATIONARY

Dec 25, 2015

MICHE 20 NA LITA 203 ZA POMBE HARAMU VYAKAMATWA KIGOMA



Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limekamata miche 20 ya bangi pamoja na lita 203 za pombe ya moshi katika Kijiji cha Kurugongo Tarafa ya Heru Chini Wilaya ya Kasulu mkoani humo bidhaa ambazo ziko kinyume na sheria.

Akizungumza na blog hii, Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, SACP Ferdinand Mtui, amesema, matukio hayo yametokea hapo jana wakati polisi wakiwa kwenye msako ambapo tukio la kwanza polisi wamemkamata Fanuel Cosmas kwa kosa la kulima miche 20 ya Bangi katikati ya shamba lake.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
 Amesema, kabla ya kumkamata mtuhumiwa polisi wamepata taarifa kutoka kwa raia wema na baada ya kufika shambani kwake wakakuta miche hiyo katikati ya shamba la mahindi.

Aidha Kamanda Mtui amesema, baada ya polisi kumkamata mtuhumiwa wa bangi, wakafanikiwa pia kuwakamata watu watano wakiwa na lita 203 za pombe ya moshi kwa malengo ya kuuza.

Hata hivyo Kamanda Mtui amewataka wananachi kuendela kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi mara wanapobaini vitendo vya kiharifu katika maeneo yao.